Wafanyabiashara wa Miraa Marsabit Central Waandamana Wakidai Kutengwa katika Programu za Uwezeshaji

MARSABIT – Wafanyabiashara wa miraa kutoka eneo la Marsabit Central, katika Eneo Bunge la Saku, Kaunti ya Marsabit, wamefanya maandamano wakieleza kutoridhishwa na kile wali…

The Signal in 30 seconds

  • MARSABIT – Wafanyabiashara wa miraa kutoka eneo la Marsabit Central, katika Eneo Bunge la Saku, Kaunti ya Marsabit, wamefanya maandamano wakieleza kutoridhishwa na kile wali…

MARSABIT –

Wafanyabiashara wa miraa kutoka eneo la Marsabit Central, katika Eneo Bunge la Saku, Kaunti ya Marsabit, wamefanya maandamano wakieleza kutoridhishwa na kile walichodai kuwa kutengwa na Serikali ya Kaunti ya Marsabit katika programu za kuwawezesha vikundi vya kijamii na kiuchumi.

Wakizungumza na wanahabari baada ya maandamano hayo, wafanyabiashara hao walisema hawakushirikishwa katika harambee ya kuchangisha fedha na kuwezesha vikundi vya jamii iliyoandaliwa katika eneo hilo. Walisema hatua hiyo imewaacha na hisia za kubaguliwa, licha ya mchango wao katika uchumi wa eneo kupitia biashara ya miraa, ambayo imekuwa tegemeo kwa familia nyingi.

Kwa mujibu wa waandamanaji, biashara ya miraa ni mojawapo ya shughuli kuu za kiuchumi katika Marsabit Central na imekuwa chanzo muhimu cha mapato kwa wafanyabiashara wengi pamoja na familia zao. Hata hivyo, walieleza kuwa sekta hiyo imeendelea kukumbwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi, zikiwemo kushuka kwa mapato na kupungua kwa uwezo wa biashara, hali ambayo imeongeza uhitaji wa kuungwa mkono kupitia programu za serikali.

Walisema kuwa, kama ilivyo kwa vikundi vingine vya kijamii vinavyonufaika na miradi ya uwezeshaji, wafanyabiashara wa miraa pia wanastahili kupewa nafasi sawa ili kuboresha biashara zao na kuinua maisha ya familia zinazozitegemea. Aidha, walisisitiza kuwa ushirikishwaji wa makundi yote ya kijamii katika mipango ya maendeleo ni muhimu kwa kuhakikisha maendeleo yanawanufaisha wananchi wote bila ubaguzi.

Waandamanaji waliitaka Serikali ya Kaunti ya Marsabit, chini ya uongozi wa Gavana Mohamud Ali, kusikiliza malalamiko yao na kuhakikisha wafanyabiashara wa miraa wanajumuishwa katika programu zote za maendeleo na uwezeshaji wa kiuchumi zinazoandaliwa na serikali ya kaunti.

Pia walitoa wito kwa viongozi wa kaunti kuanzisha mazungumzo ya wazi na wawakilishi wa wafanyabiashara wa miraa ili kujadili changamoto zinazowakabili na kutafuta suluhu ya kudumu kuhusu ushirikishwaji wao katika miradi ya maendeleo.

Walisema mazungumzo hayo yatasaidia kujenga uhusiano mzuri kati ya serikali na wafanyabiashara, pamoja na kuhakikisha kuwa kila kundi linapata fursa sawa za kunufaika na mipango ya maendeleo, pamoja na kubuni mbinu sahihi itakayosaidia katika kuboresha biashara hii ambayo ndio chanzo kikuu cha wakazi wa eneo hilo.

Hadi kufikia wakati wa kuchapishwa kwa taarifa hii, Serikali ya Kaunti ya Marsabit ilikuwa haijatoa tamko rasmi kuhusu madai yaliyotolewa na wafanyabiashara hao.

Share this story

About the author

J

JB Nateleng

Kenya Signal Room Contributor

I am a Kenyan journalist, radio and television presenter, public relations practitioner, and storyteller based in Marsabit County. I am passionate about delivering accurate, impa…

View author profile

Corrections & updates

Kenya Signal Room corrects factual errors promptly. To request a correction, contact the editorial team through our contact page.

Stay in the Signal

Get the morning brief: 5 stories, 1 explainer, and the county signal to watch.

Know something we should investigate?

Send a verified tip, document, photo or story idea to Kenya Signal Room.

Submit a Tip

Comments

No approved comments yet. Be the first to join the conversation.

Comments appear after admin approval.