Wakazi wa Dukana Waandamana Kupinga Huduma Duni za Afya

DUKANA, MARSABIT  Wakazi wa eneo la Dukana, Kaunti ya Marsabit, wameandamana kupinga kile walichokitaja kuwa huduma duni katika Kituo cha Afya cha Dukana, wakitaka Serikali y…

The Signal in 30 seconds

  • DUKANA, MARSABIT  Wakazi wa eneo la Dukana, Kaunti ya Marsabit, wameandamana kupinga kile walichokitaja kuwa huduma duni katika Kituo cha Afya cha Dukana, wakitaka Serikali y…

DUKANA, MARSABIT

Wakazi wa eneo la Dukana, Kaunti ya Marsabit, wameandamana kupinga kile walichokitaja kuwa huduma duni katika Kituo cha Afya cha Dukana, wakitaka Serikali ya Kaunti ya Marsabit na Serikali ya Kitaifa kuchukua hatua za haraka kuboresha utoaji wa huduma za afya.

Maandamano hayo yaliwashirikisha vijana, wanawake, wazee na viongozi wa jamii waliobeba mabango yenye ujumbe wa kutaka wahudumu zaidi wa afya kupelekwa katika kituo hicho. Waandamanaji walieleza kuwa kwa muda mrefu kituo hicho kimekuwa kikikumbwa na upungufu mkubwa wa wahudumu wa afya, hali ambayo imeathiri utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa mujibu wa wakazi, wagonjwa hulazimika kusubiri kwa saa nyingi kabla ya kuhudumiwa kutokana na idadi ndogo ya wahudumu waliopo. Walisema hali hiyo imekuwa changamoto kubwa kwa makundi yaliyo katika mazingira hatarishi, hususan wanawake wajawazito, watoto na wazee wanaohitaji matibabu ya haraka. Pia walieleza kuwa baadhi ya wagonjwa hulazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za matibabu katika maeneo mengine kutokana na ukosefu wa huduma za kutosha Dukana.

Viongozi wa jamii walioungana na waandamanaji walisema kuwa afya ni haki ya msingi ya kila mwananchi na kwamba wakazi wa Dukana wanastahili kupata huduma bora kama ilivyo katika maeneo mengine ya nchi. Walitoa wito kwa Serikali ya Kaunti ya Marsabit kuajiri wahudumu zaidi wa afya, kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wakati na kuboresha miundombinu ya kituo hicho ili kiweze kukidhi mahitaji ya idadi inayoongezeka ya wakazi.

Kufuatia malalamiko hayo, Serikali ya Kaunti ya Marsabit imetangaza mipango ya kuajiri wahudumu zaidi wa afya ndani ya wiki mbili zijazo ili kukabiliana na upungufu wa wafanyakazi katika vituo vya afya vya umma.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, waziri wa afya Malicha Boru, amesema zoezi la uajiri linalenga kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa kuongeza idadi ya wahudumu katika hospitali na vituo vya afya vinavyokabiliwa na uhaba wa wafanyakazi.

Malicha pia alisema serikali ya kaunti inaendelea na mchakato wa ununuzi wa dawa na vifaa tiba vya ziada vitakavyosambazwa katika hospitali na vituo vya afya kote kaunti ili kuboresha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi.

Waandamanaji walikaribisha tangazo hilo lakini wakasisitiza kuwa wanatarajia hatua hizo kutekelezwa kwa haraka. Walisema wataendelea kufuatilia utekelezaji wa ahadi hizo ili kuhakikisha wakazi wa Dukana wanapata huduma bora za afya wanazostahili.

Hadi kufikia wakati wa kuandaa taarifa hii, wakazi walieleza matumaini kuwa hatua zilizotangazwa na Serikali ya Kaunti ya Marsabit zitasaidia kupunguza changamoto za upungufu wa wahudumu wa afya na kuboresha huduma katika Kituo cha Afya cha Dukana.

Share this story

About the author

J

JB Nateleng

Kenya Signal Room Contributor

I am a Kenyan journalist, radio and television presenter, public relations practitioner, and storyteller based in Marsabit County currently working with Radio Jangwani Marsabit as…

View author profile

Corrections & updates

Kenya Signal Room corrects factual errors promptly. To request a correction, contact the editorial team through our contact page.

Stay in the Signal

Get the morning brief: 5 stories, 1 explainer, and the county signal to watch.

Know something we should investigate?

Send a verified tip, document, photo or story idea to Kenya Signal Room.

Submit a Tip

Comments

No approved comments yet. Be the first to join the conversation.

Comments appear after admin approval.